STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 27, 2013

UNYAMA! Baba awauwa wanae wawili Kigoma, kisa mibangi!

Mauaji dhidi ya watoto kila kona. Hapa ni mwili wa mtoto Ayoub Agen ulipokuwa ukienda kuzikwa baada ya kuuwawa kinyama huko Rungwe mkoani Mbeya hivi karibuni. Watoto watafanyilia ukatili kama huo mpaka lini?
MATUKIO ya kikatili dhidi ya watoto wasio na hatia yamezidi kuendelea safari hii watoto wawili wachanga wamejikuta wakiuwawa kikatili na baba yao mzazi ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kwa mauaji hayo yaliyotokea juzi asubuhi katika kijiji cha Mvugwe wilayani Kasulu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kigoma, Fraiser Kashai, unyama huo ulifanywa na Majuto Thobias, 27 Jumatano asubuhi kwa kuwauwa watoto wake mwenyewe, mmoja akimchoma kisu na mwingine kichanga cha miezi mitatu kwa kumbamiza sakafuni na kumtoa uhai.
Kamanda huyo alisema majuto alimchoma kitu Loyce Majuto mwenye miaka miwili kifuani na kukishindilia hadi alipokata roho kabla ya kumgeukia kichanga kingine kilichokuwa kitandani chenye miezi mitatu kikiwa hakina jina bado na kumbamiza chini mara tatu hadi alipokufa.
Inaelezwa kuwa wakati mwanaume katili akifanya unyama huo, mkewe alikuwa nje akipika na aliposikia vilio vya wanae alikimbilia ndani na kukumkuta mtuhumiwa huyo akifanya ukatili huo kwa watoto wao.
Kamanda alisema mwanamke huyo aliamua kupiga mayowe kuita majirani baada ya kuwashuhudia wanawe wakiuwawa kikatili na ndipo walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha kituo cha Polisi.
"Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo ambaye tunamshikilia alifanya ukatili huo kwa watoto wake kutokana na kile kinachoelezwa kuwa mtumiaji sugu wa dawa za kulevya aina ya bangi na kwamba upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea kufanyika kabla ya kumfikisha mahakamani kwa makosa yanayomkabili" alisema.

No comments:

Post a Comment