STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 27, 2013

Serikali yawakumbuka wanyonge


Na Suleiman Msuya
SERIKALI kupitia Wizara ya Sheria na Katiba ipo katika mchakato wa kutunga sheria ya Msaada wa Kisheria ambayo inalenga kuwasaidia wananchi na uwezo wa kulipia gharama zinazotozwa na Mawakili wa kujitegemea.
Hayo yamebainishwa Msemaji wa Wizara hiyo Farida Khalfan wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema Wizara ya Sheria mwaka 2010 iliiunda kikosi kazi ambacho kilishirikisha wadau mbalimbali kufanya utafiti na kutoa mapendekezo juu ya mfumo sahihi ambao utakidhi hitaji kwa kila raia.
Msemaji huyo alisema baada ya kikosi kazi hicho kuwasilisha mapendekezo s.erikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria ilianza utaratibu wa kutunga sheria itakayojulikana kama (Sheria ya Msaada wa Kisheria)
Khalfan alisema maandalizi ya sheria hiyo yapo katika hatua za mwisho ambapo matarajio yao ni kuhakikisha kuwa sheria hiyo inawasilishwa Bungeni ifikapo Januari mwaka 2014.
“Tumekuwa tukifuatilia changamoto ambazo zinawakuta wananchi hasa katika masuala ya kisheria ila kutokana gharama kubwa ila tunaaamini kuwa mwakani utatuzi utakuwa ukipatikana,” alisema.
Alisema katika sheria hiyo itaunda chombo huru kitakachokuwa na majukumu mbalimbali ambayo ni kusajili taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, kusajili watoa msaada wa kisheria, kuweka ubora wa viwango katika utoaji msaada wa kisheria na kuvisimamia.
Khalfan alisema pia chombo hicho kitasimamia nidhamu na maadili ya watoa huduma za msaada wa kisheria, kutambua wasaidizi wa kisheria na kutafuta fedha ili kutekeleza majukumu yake.
Alisema matoke ya kuwepo kwa sheria hiyo ni dhahiri kuwa watoa msaada wa kisheria atatakiwa kusajiliwa ili waweze kutoa huduma hiyo kupitia vituo vilivyosajiliwa kutoa msaada huo.
Msemaji huyo alisema kukosekana kwa sheria hiyo ndio sababu mojawapo ya kuwepo kwa watu wasio na sifa za kutoa huduma hiyo ambao wanatambulika kama (Bush Lawyers) ambao wamekuwa wakiwarubuni wananchi kuwa wanaweza kuwasaidia kisheria.
Alisema kupita kwa sheria hiyo kutasaidia jamii mbalimbali kama watoto, wajane na watu wote ambao wamekuwa wakipata shida ya msaada wa kisheria nchini kutokana na gharama kubwa zinazotozwa na wanasheria .

No comments:

Post a Comment