STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 27, 2013

Lissu aponda uendeshaji wa Bunge, adai unakwamisha mengi ya maana

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh7-RqMhZYObN7yssSphvShWb4-noohMWpS-9fKfjYq9-a2R7Xz-srjovqDZ9GotCSbrnW7vv17aUlo9XPnNVAjodYGYnPkKGQSWQYzKhmMcl2bkgMEK3xC49D9gnIOeqlhXBydAVfiM8KX/s320/tundu+lissu.jpg
Tundu Lissu akiwa Bungeni
Na Suleiman Msuya
MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini Tundu Lissu amesema itakuwa maajabu kwa wabunge wa Bunge la sasa kufanya maajabu kutokana na mfumo wa uendeshaji wake.
Lissu alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akichangia katika kongamano linaloratibiwa na taasisi ya  Jukwaa la Jamii (Policy Forum) kila mwisho wa mwezi.
Alisema kumekuwepo na dhana kuwa wabunge ndio wanaweza kufanya maamuzi katika masuala ya kitaifa lakini kusema ukweli mfumo wa uendeshaji wake itakuwa jambo gumu kwa sasa.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema ili Bunge hilo liweze kuwa na tija ni wakati muafaka kwa wananchi kufanya maamuzi sahihi pindi wanapopatiwa fursa hiyo.
“Jamani Watanzania napenda kuwaambia kuwa kwa mfumo wa Bunge hili la sasa wasitarajie kutokea maajabu kwani inabidi iwe hivyo ila wakati wa kufanya mabadiliko unakaribia,” alisema.
Lisu alisema dhana ya kuwa uchangiaji wa wabunge kuonekana wa mashaka unachangiwa na elimu alikanusha suala hilo na kusema mfumo mzima ndio chanzo cha matatizo hayo hivyo ni vema wananchi wakawa na subira ili kuhakikisha kuwa mabadiliko yanatokea.
Alisema elimu sio sababu ya kuonekana kwa uwezo mdogo kutokana na ukweli kuwa hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kuwa mjuzi wa kila jambo.
Mbunge huyo alisema wabunge wengi hawana ofisi jambo ambalo linachangia kufanya kazi hata wakiwa baa hali ambayo haiwezi kuleta tija kwa maslahi ya nchi.
Alisema kumekuwepo na changamoto kubwa juu ya nguvu ya maamuzi kati ya Bunge na Serikali hali ambayo inachangia upande mmoja kujiona ndio wenye sifa ya kufanya maamuzi ya mwisho.
Lisu alisema Bunge limekuwa likinyimwa nafasi kutokana na dhana kuwa iwapo watakuwa na msimamo juu yabhoja Fulani ni dhahiri kuwa upo uwezekano wa Bunge kuvunjwa ambapo wabunge waliowengi wanaamini kuwa wanaweza wasirudi baada ya uchaguzi.
Kwa upande wake Mbunge wa Kisesa Luhanga Mpina alisema mfumo wa kuwasilisha bajeti bado unachangamoto nyingi ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuhakikishakuwa bajeti inaleta tija kwa jamii.
Mpina alisema kumekuwepo na tabia ya kuwasilisha vitu nusu nusu wakati bunge likiendelea na vingine kutowasilishwa jambo ambalo linatia shaka juu ya nini kinafichwa katika mchakato huo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa ofisi ya Bunge ya bajeti, kutopatikana kwa vitabu vya mapato, uwazi juu ya matumizi ya misaada, taarifa za mkaguzi na zinginezo nyingi.
Mbunge huyo ambaye amekuwa na msimamo wa kujiamini pindi anapochangia hija zake Bungeni alisema ni vema kukawa na uwazi juu ya masauala ya katiba, uelewa na kuhakikisha kuwa wabunge wanashiriki kikamilifu tangu awali.

No comments:

Post a Comment