STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, July 27, 2013

Serikali yaja na mikakati ya kuibua ajira 30,000 kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjH1bttKwptQaUumeTy5iQpTKX7qhgREzLaMpw_UjLldbYRkqeqi-I2EdgvtaLiMtAs04sNUGZBslW7C-tAE2PTEM0dxDbjDjE4XhZ78Jo0YZj9pO9h5YJiDKO3hNefCFXpxp64lVotQ-JE/s400/Waziri+wa+Kazi+na+Ajira+Bi.+Gaudentia+Kabaka.JPG
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka

Na Suleiman Msuya
WIZARA ya Kazi na Ajira ipo katika mkakati wa kuanzisha programu ambayo itahusisha vijana waliomaliza vyuo vikuu na kuweza kuzalisha ajira 30,000 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo Ridhiwan Wema wakati akizungumza na mwandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Alisema programu hiyo itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini, taasisi za fedha na wabia wa maendeleo mbalimbali.
Wema alisema kwa kuanzia wake utaanza kwa kuendeleza programu ya mfano iliyoanzishwa na Idara ya kilimo, uchumi na biashara katika Chuo Kikuu cha Sokoine (DAEA-SUA) na hatimaye kuwafikia wahitimu wa vyuo vingine vya elimu ya juu.
Msemaji huyo alisema kwa kuanzia Serikali imekubaliana na Benki ya CRDB kuanzia utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa programu utakapoanza.
“Tumekuja na programu mpya ambayo tunatarajia kuwa itaweza kuzalisha ajira 30,000 baada ya miaka mitatu na itagharimu shilingi bilioni 54.451 kwa kuhusisha vijana wa vyuo vikuu nchini wanaomaliza kwani takwimu zinaonyesha kila mwaka ni asilimia 48,” alisema.
Alisema madhumuni ya programu hiyo ni katika utekelezaji wa sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 ya kuhamasisha uzalishaji wa kitaifa kufanikisha ajira kalimi  yenye kipato.
Wema alisema lengo la programu hiyo ambayo inahusisha vijana ni kuhakikisha kuwa vijana zaidi ya laki moja (100,000) wanapata ajira kupitia hatua mbalimbali kulingana na sifa zao.
Msemaji huyo pia lengo hilo ni kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki shughuli rasmi za kiuchumi na wamejiajiri na kuajiri wengine, kukuza utamaduni wa kijasiriamali pamoja na ubunifu na kuhamasisha matumizi bora ya nguvu kazi.

No comments:

Post a Comment