Na Dina Ismail
BAADA ya kuipiga danadana kwa
muda mrefu, hatimaye klabu ya soka ya Yanga imemgeuzia kibao aliyekuwa kiungo
mshambuliaji wake wa kimataifa,Hamis Kiiza.
Hivi karibuni nyota huyo
kutoka nchini Uganda, amekuwa katika mvutano na uongozi wa klabu hiyo juu ya
kusaini mkataba mpya wa kuendelea kutumikia klabu hiyo.
Kwamba, Kiiza alitaka
kuongezwa ofa ya aliyopewa na uongozi kutoka dola 35,000 hadi dola 50, 000
ambazo amesisitiza kupewa na baadaye kumuongeza hadi dola 40,000.
Hata hivyo, habari kutoka
ndani ya uongozi wa Yanga zinaeleza kwamba wameamua kuachana kwanza na suala la
Kiiza kutokana na nafasi yake kutokuwa na umuhimu katika kikosi hicho.
Kiongozi mmoja aliliambia
gazeti hili kwamba kwa sasa Yanga inahitaji mshambuliaji halisi mmoja ambaye
atashirikiana na mshambuliaji aliyepo sasa, Didier Kavumbagu.
“Kwa sasa suala la Kiiza
tumeliweka kando kwani nafasi yake haina umuhimu katika kikosi chetu,
tunatafuta mshambuliaji halisi, ila tukikosa ndo tutarudi kwake,”alisema
Akienda mbali zaidi, kiongozi
huyo alisema kwamba mshambuliaji huyo anafahamu kila kitu juu ya mustakabali
wake ndani ya klabu hiyo na hata hilo suala la kumpa fedha anayoitaka yeye
halipo.
Aliongeza kuwa baada ya
kumleta mshambuliaji kutoka Nigeria Ogbu Brendan kwa ajili ya majaribio, hivi karibuni tena
wanataleta washambuliaji wengine kuja kujaribiwa.
Katika hatua nyingine, kikosi
cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania
Bara ambapo keshokutwa itacheza mechi ya kirafiki na URA ya Uganda.
Mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukipima kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment