MPIGANIA Haki za mashoga nchini Cameroon amekutwa amekufa nyumbani kwake Yaounde
baada ya kuteswa, Wapigania Haki za Binadamu wamesema.
Mwili
wa Eric Lembembe ulikutwa kwenye jiji hilo mnamo siku ya Jumatatu huku
ukionekana alikuwa ameteswa vibaya sana, kundi hilo lilisema kwenye
maelezo yao siku ya Jumanne.
“Marafiki
wa Lembembe waliukuta mwili wake mnamo siku ya Jumatatu jioni. Kwa
mujibu wa rafiki zake shingo yake ilivunjwa na uso wake, mikono na miguu
viliunguzwa moto kwa kutumia pasi,” taarifa ilisema.
Shirika hilo limeelezea kitendo hicho kama ni cha “mauaji”na kuzitaka mamlaka husika kuendelea kufanya uchunguzi wa kina.