Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani
Tanzania, Bernard Luanda kuongoza Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kufuatia
mabadiliko ya Katiba yaliyofanywa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) na
kuingiza kamati nyingine mpya.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga ametangaza wajumbe wa kamati hizo jana (Julai 18
mwaka huu) mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF
kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema
uteuzi wa wajumbe hao umezingatia maoni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
TFF, lakini vilevile amewashukuru wajumbe walioteuliwa kwa kukubali
kutoa mchango wao katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mbali
ya Jaji Luanda ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, wajumbe ni Francis
Kiwanga (Makamu Mwenyekiti), Anney Semu, Yohane Masalla na Allen
Kasamala. Kamati ya Uchaguzi inaongozwa na Hamidu Mbwezeleni, Moses
Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Mustafa Siyani, Hassan Dyamwale na Kitwana
Manara.
Mwenyekiti
Kamati ya Rufani ya Maadili ni Jaji Steven Ihema, Bi. Victoria Makani
(Makamu Mwenyekiti), Mheshimiwa Mohamed Missanga, Henry Tandau na
Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Kamati ya Maadili inaundwa na Bi. Jesse
Mguto (Mwenyekiti), Francis Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Profesa Mtambo
Madundo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga na Evod Mmanda.
Profesa
Mgongo Fimbo anaongoza Kamati ya Rufani ya Nidhamu wakati Makamu wake
ni Ong’wanuhama Kibuta na wajumbe ni Kanali Mstaafu Idd Kipingu, Dk.
Mshindo Msolla na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mstaafu
Jamal Rwambow. Kamati ya Nidhamu inaongozwa na Kamishna wa Polisi (CP)
Mstaafu Alfred Tibaigana, Mustafa Kambona (Makamu Mwenyekiti),
Mheshimiwa Azzan Zungu, Yusuf Nzowa na Mohamed Msomali.
Pia
Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko katika Kamati ya Waamuzi ambapo
Said Nassoro na Charles Ndagala kutoka Chama cha Waamuzi wanachukua
nafasi za Joan Minja na Riziki Majala. Kamati hiyo inaendelea kuongozwa
na Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge, Omar Kasinde (Makamu Mwenyekiti)
wakati mjumbe mwingine ni Mohamed Nyama.
Kamati
ya Tiba inaongozwa na Dk. Paul Marealle wakati nafasi ya Makamu
Mwenyekiti itajazwa baadaye na Rais Tenga. Wajumbe ni Mwanandi
Mwankemwa, Anthony Ngome, Frank Mhonda, Kapteni Joakim Mshanga na Helen
Semu.
Rais
Tenga alisema mabadiliko mengine yamefanyika kutokana na waliokuwa
wajumbe kuomba kupumzika. Wajumbe walioomba kupumzika ni Dk. Sylvester
Faya, Idd Mtiginjola na Deo Lyatto
No comments:
Post a Comment