Mwili wa Erasto Msuya baada ya kupigwa risasi.
IKIWA ni takribani siku tatu zimepita tokea mfanyabiasha wa madini ya Tanzanite na mmiliki wa hotel kitali ya S.G Resort iliyopo jijini Arusha
aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi 21 na
kumsababishia kifo papo hapo katika eneo la njia panda ya KIA wakati
akitoka Mirerani kuelekea Arusha mjini majira ya mchana.
Habari kutoka katika kamati ya mazishi inayoundwa na
wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite, ikiongozwa na kaka mkubwa marehemu
Gady Msuya, anasema zaidi ya shilingi milioni mia moja (100,000,000/=) inatarajiwa kutumika kugharamia mazishi
ya mfanyabiashara huyo bilionea wa madini yav Tanzanite. Na kaka wa Marehemu (Gady) aliendelea kusema kuwa gari maalumu la kubeba mwili wa marehemu na jeneza
vimeagizwa kutoka Nairobi, nchini Kenya kwa gharama ya Shilingi milioni nane (8,000,000/=).
Kiasi hicho cha zaidi ya milioni mia moja kinarajiwa kuchangwa na
wafanyabiashara wenzake wa madini . Pia wanatarajia kulipia
magari maalumu yatakayotumika kwenye msafara wa mazishi ya Erasto Msuya
yanayotarajiwa kufanyika nyumbani kwake Mirerani, wilayani Simanjiro siku ya jumanne ya tarehe 13 August 2013.
No comments:
Post a Comment