Na Suleiman Msuya
WAKATI jamii ya Kitanzania ikiwa imeelekeza mitazamo,
michango na mawazo juu ya aina ya Katiba ambayo wanaitaka Jumuiya ya Wanafunzi
wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) wamependekeza kuwepo kwa haki ya
kupatiwa elimu bora, haki za wanaume pamoja na kuomba suala la muungano liwe la
wananchi wote kutoa maoni.
Hayo yamebainshwa na Mwenyekiti wa TAHLISO Amon
Chakushemeire wakati akizungumza na MICHARAZO, ambapo alisema mapendekezo hayo yametokana baraza wa
wanachama wa TAHLISO ambao walikutana Mkoani Mbeya kwa siku mbili ambapo waliweza
kujadili rasimu ya Katiba wakiwa sehemu ya baraza.
Mwenyekiti baada ya kuipitia kwa undani rasimu hiyo wajumbe
waligundua mambo makuu matatu ambayo ni haki ya kupatiwa elimu, haki za wanaume
na muundo wa muungano ndiyo yanahitaji kuwekwa kama mapendekezo baada ya kuona
watu wengi wamekuwa wakiyajadili mambo mengine na kuyaacha.
“Unajua watu wengi waliochangia rasimu ile
wameonekana kusauhau suala la haki ya kupatiwa elimu, haki za wanaume jambo
ambalo linaonekana kuwa linaweza kufanya yakasahaulika na kuendelea kuleta
athari kwa jamii,” alisema.
Alisema suala la elimu linahitaji kubainishwa kwenye
katiba moja kwa moja ili kuhakikisha kuwa jamii inapatiwa elimu kuanzia msingi
hadi mahali ambapo mfaidika ataweza kutumikia jamii.
Chakushemeire alisema suala la kuwepo kwa haki za
wanaume linaonekana kama halina tija ila ukweli ni kwamba jamii ya wanaume
imekuwa ikipata athari kubwa ila haina pahali pa kusemea.
Mwenyekiti huyo alisema suala la muundo wa muungano
ni vema likarejeshwa kwa wananchi ili waweze kufanya maamuzi wao wenyewe na
lisiwe ni suala la watu wachache.
Akizungumzia suala la TAHLISO kuhusishwa na
kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea nafasi za Urais Katibu wa TAHLISO Donati
Salla alisema wao hawahusiki na mambo hayo na kuwataka wanachama wao kutotumia
nembo yao kufanya mambo yao binafsi.
Salla alisema wanaotajwa kuwa walikuwa viongozi wa
TAHLISO huko morogoro ni kweli kuwa ni wanachama TAHLISO ila hakutumwa na wao
na ni watu wenye maslahi yao binafsi jambo ambalo wanalipinga.
Aidha alitoa angalizo kwa baadhi ya watu ambao
wanajiita Taasisi ya Vijana Tanzania (TAVITA)
kuacha kuwashirikisha wanachama wa TAHLISO katika mikakkati yao ya kutumiwa na
watu wenye mipango ya kugombea Urais mwaka 2015.
Alisema kundi hilo linatarajiwa kukutana Septemba 7
mwaka huu nyumbani kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu wilayani Monduli.
No comments:
Post a Comment