Na Suleiman Msuya
THAMANI ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikali
imekuwa kutoka bilioni 72.55 mwaka 2008/2009 hadi kufikia bilioni 178.3 mwezi
Juni mwaka 2013.08.30
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa GEPF Festo
Fute wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema ongezeko hilo limechangiwa na kuongezeka kwa
wanachama pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali kama amana za serikali, makampuni yaliyo orodheshwa
kwenye soko la mitaji (DSE), uwekezaji wa muda maalum kwenye mabenki ya
biashara, mikopo, hati fungani na majengo.
Fute alisema hadi kufikia mwaka huu GEPF imefanikiwa
kusajili wanachama 60, 030 ambapo kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 walikuwa
wanachama 30,227 hiyo ikitokana na
jitihada zao za kuhakikisha kuwa watu wote wanafaidika na mfuko huo.
“Unajua katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii moja
ya malengo yake ni kuhakikisha kuwa thamani ya mfumo inaongezeka jambo ambalo
tumeweza kulitekeleza kwani sasa mfumo una thamani ya shilingi bilioni 198.30,”
alisema.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema vitegauchumi wa mfuko
viliongezeka kutoka shilingi bilioni 64.94 mwaka 2009 hadi kufikia shilingi
179.68 mwaka 2013, ambapo na mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 5.48 mwaka 2009 hadi
bilioni 18.25 mwaka 2013.
Alisema pamoja mafanikio hayo ya thamani ya mfuko
ila pia wamekuwa wakiwalipa wanachama wao mafao kwa wakati ambao kwa kipindi
cha mwaka 2012 hadi 2013 zaidi ya bilioni 5 zimelipwa kwa wanachama kama mafao.
Aidha akizungumzia kuhusu mpango wa hiari wa
kujiwekea akiba ya uzeeni (VSRS) alisema mfuko huo umekuwa na mafanikio makubwa
ambapo tangu mwaka 2009 hadi 2013 wameweza kusajili na wanachama 18,700 ambapo
jumla ya akiba za wanachama zilifikia kiasi cha shilingi bilioni 3.05.
Fute alisema katika mfuko huo wanachama
wamegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ni wafanyabiashara 7,480, kilimo
ufugaji 6,545, ujasiriamali 1,683 na waajiriwa 2,992.
Pia alisema pamoja na mafanikio ambayo wameyapata
pia mfumo huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama kupitwa kwa sheria
inayoongoza mfuko na ufahamu mdogo wa watu kuhusu mfuko.
No comments:
Post a Comment