STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 25, 2014

Babi aianza vyema Ligi ya Malaysia UiTM yashinda ugenini

Abdi Kassim akiwa na wachezaji wenzake baada ya gemu yao ya jana
KIUNGO Abdi Kassim 'Babi' aliiongoza vyema klabu yake ya UiTM ya Malaysia kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kuala Lumpur SPA katika mechi za fungua dimba ya  Ligi Kuu ya nchi hiyo iliyoanza rasmi jana.
UiTM ikiwa ugenini ilipata ushindi huo ikiwa ni siku chache baada ya kunyukwa mabao 3-2 katika michuano ya FA, huku Babi akihusika na mabao yote ya timu yake.
Akizungumza na MICHARAZO toka Malaysia, Babi alisema pambano hilo la jana lilikuwa gumu na lenye ushindani na wanashukuru kuanza kwa ushindi katika ligi hiyo na kuifanya timu yao ikamate nafasi ya tano kwenye msimamo huo.
Babi alisema kikosi chao kinatarajiwa kushuka tena dimbani Jumatatu dhidi ya timu ya Johor pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Mini UiTM.
Katika mechi nyingine za fungua dimba za Ligi Kuu ya Malaysia, Felda United ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na PBAPP, Negeri Sembilan iliishindilia DRB-Hicom kwa mabao 2-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani, huku Kedah ikiwa nyumbani kuisasambua Perlis kwa mabao 4-1, Johor ilala nyumbani kwa mabao 3-1 kipigo walichopewa na PDRM na Pulau Pinang ilipata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Sabah.
No comments:

Post a Comment