STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 25, 2014

Nigeria yaiduwaza Morocco, ikitinga nusu fainali CHAN 2014

http://en.starafrica.com/football/files/2014/01/B14AKCR14441.jpg
TIMU ya soka ya Nigeria imeiduwaza Morocco baada ya kuing'oa kwenye michuano ya CHAN 2014 baada ya kuifunga mabao 4-3 katika muda wa dakika 120 ya pambano la kwanza la Robo Fainali  ya kwanza kwenye uwanja wa Cape Town.
Nigeria iliyoonekana kama inaondoka kwenye michuano hiyo ililazimisha mchezo huo kwenda kwenye dakika hizo baada ya kuchomoa bao dakika za lala salama za dakika 90 na kufanya matokeo kuwa 3-3 na kuongezewa dakika 30 zilizowapa ushindi.
Katika muda wa dakika 90,  Morocco walitangulia mabao yake yake matatu  katika kipindi cha kwanza kupitai kwa Moutouali aliyefunga mawili katika dakika ya 33 na 40, Iajour dakika ya 37.
Kipindi cha pili Nigeria ilitulia na kuanza kurejesha bao moja baada ya jingine kupitia kwa  Uzochukwu aliyefunga dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi hicho kabla ya Ali kuongeza la pili dakika ya  55 na Uzoenyi kusawazisha dakika ya 90 na kufanya mchezo kuongezwa dakika 30.
Katika muda huo wa nyongeza, Nigeria ilipata bao lake lililoivusha hadi nusu fainali ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tatu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, liliwekwa kimiani na Abubakar Ibrahim katika dakika ya 111.
Robo fainali ya pili ya michuano hiyo inatarajiwa kuanza hivi punde kwa pambano kati ya Zimbabwe dhidi ya Mali mchezo utakaochezwa uwanja huo huo wa Cape Town.

No comments:

Post a Comment