STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 25, 2014

Duru la pili laanza kwa kishindo, Yanga yaiua tena Ashanti

Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Ashanti United katika mechi yao ya leo Taifa
Mbeya City na Kagera Sugar kabla ya pambano baina yao

Coastal Union ilipokuwa ikiumana na Oljoro uwanja wa Mkwakwani Tanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imedhihirisha haikwenda Uturuki kutalii baada ya kuinyuka Ashanti United kwa mabao 2-1, huku wazee wa Oman, Coastal Union ya Tanga ikijikuta ikilazimishwa sare ya 1-1 na Oljoro JKT katika mechi za fungua dimba la duru la pili la Lligi hiyo.
Yanga ilikwaruzana na Ashanti kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kipindi cha kwanza kiliisha bola timu hizo kushindwa kufungana.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa dakika ya 51 Didier Kavumbagu akimalizia pasi ya Simon Msuva aliyegongeana na Haruna Niyonzima, hata hivyo dakika chache baadaye Ashanti walirejesha bao hilo kupitia Mnigeria Dayton Obinna.
David Luhende aliyepamba mbele aliihakikishia Yanga ushindi wa mabao 2-1 baada ya kufunga bao la pili kwa shuti la karibu ndani ya lango ya Ashanti katika dakika ya 79.
Kwa ushindi huo Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni kwa kufikisha pointi 31 ikifuatiwa na Azam ambayo ilianza duru hilo kwa kishindo kwa kuilaza Mtibwa Sugar mabao 1-0 katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Bao hilo pekee liliwekewa kimiania na Kipre Tchetche akimalizia kazi ya Joseph Kimwaga na kuendeleza rekodi yao ya kutopotea mechi kwenye ligi hiyo na kuzidi kuipumulia Yanga kileleni ikitopfautiana nao kwa pointi moja tu.
Nayo Mbeya City iliendeleza rekodi yao ya kushinda kokote inapoenda kucheza kwenye ligi hiyo baada ya kuiduwaza Kagera Sugar kwa kuilaza bao 1-0 uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Katika mechi nyingine ya leo kwenye ligi hiyo iliyochezwa mjini Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, Coastal iliyokuwa Oman ikijifua ilishindwa kulinda bao lao baada ya Oljoro JKT kusawazisha bao dakika za jioni ya kuzifanya hivyo hizo zigawane pointi moja moja.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili Simba kuikaribisha Rhino Rangers ya Taboira kwenye uwanja wa Taifa na JKT Ruvu kuialika Mgambo JKT kwenye uwanja wa Chamazi.

No comments:

Post a Comment