STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 14, 2014

Coastal yaendelea kutoa vipigo OmanMABINGWA wa zamani wa soka nchini Tanzania, Coastal Union imeendelea kutoa dozi ya vipigo kwa wenyeji wao nchini Oman baada ya jioni ya leo kuilaza kwa mabao 2-0 Oman Club ikiwa ni ushindi wake wa pili mfululizo tangu watue nchini huyo kwa kambi ya mazoezi ya wiki mbili.
Awali Coastal iliinyoa kwa idadi kama hiyo timu ya Al Mussanah mabao yaliyofungwa na Yayo Kato na Kenneth Masumbuko.
Katika mechi ya leo iliyochezwa kwenye uwanja wa Nadi Oman katika wilaya ya Boshra jijini Muscat.
Magoli ya Coastal katika mechi hiyo yaliwekwa kimaini na Mohammed Miraji dakika 35, na Yusuf Chuma dakika 75.
Kikosi hicho kinachonolewa na Mkenya Yusuf Chipo kinatarajiwa kucheza mechi nyingine mbili ikiwa nchini humo chini ya uenyeji wa Fanja Fc tangu Januari 9. mechi hizo zitahusisha timu za Seeb Club na Fanja Club,zilizopo Ligi Kuu ya nchi hiyo. Oman Club yenyewe inashiriki Ligi daraja la Kwanza.

No comments:

Post a Comment