STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 14, 2014

Arsenal mbele kwa mbele yarejesha kileleni ikilipa kisasi kwa Villa

Kitu!
Werawera mwanawaneee!
VIJANA wa Arsene Wenger wamezidi kuonyesha dhamira yao ya kunyakua taji la Ligi kuu ya England baada ya usiku wa jana kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kuitambia Aston Villa ikiwa kwao kwa kuicharaza mabao 2-1.
Ushindi huo umeifanya Arsenal kuchupa toka nafasi ya tatu iliyokuwepo baada ya Chelsea na Manchester City kuiporomosha na kupokezana kwa muda uongozi wa ligi hiyo mwishoni mwa wiki kwa kufikisha poiinti 48, moja zaidi ya City yenye 47 na mbili zaidi ya Chelsea iliyokusanya pointi 46.
Mabao yaliyoihakikishia Arsenal kurejea kileleni yalifungwa na Jack Wilshere alifunga dakika ya 34 na Olivier Giroud akaongeza la la pili dakika ya 35 na kluifanya vijana hao wa London ya Kaskazini kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilikuwa cha wenyeji kuweza kujipatia bao pekee la kufutia machozi lililofungwa na nyota wao  Cristian Benteke katika dakika ya 76 na kuifanya Arsenal kuvuna pointi tatu na pia kulipa kisasi cha kunyukwa na Villa katika mechi yao ya duru la kwanza kabla ya vijana hao wa Wenger kuzinduka.

No comments:

Post a Comment