STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 14, 2014

Ethiopia yashindwa kuhimili vishindo vya Libya CHAN 2014

Ethiopia
Libya
WAWAKILISHI wa ukanda wa Afrika Mashariki na Ethiopia jana ilianza vibaya michuano ya CHAN-2014 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Libya katika pambano la kundi C lililochezwa kwenye uwanja wa Free State, Bloemfontein.
Ethiopia wanakamata nafasi ya pili katika ubora wa viwango vya soka kwa nchi za CECAFA nyuma ya Uganda ambayo juzi ilianza kwa kuipa kipigo Burkina Faso walishindwa kuhimili vishindo vya waarabu na kujikuta wakifungwa bao la mapema katika dakika ya nne tu ya kuanza kwa pambano hilo.
Bao hilo liliwekwa kimiani na Elmutasem Abushnaf na kudumu hadi wakati wa mapumziko na kwenye kipindi cha pili Ethiopia waliwabana Libya na kuonyesha dalili za kurejesha bao hilo kabla ya kujikuta wakiruhusu tena bao la pili katika dakika ya 83 lililofungwa na Abdulsalam Omar akimalizia kazi nzuri ya Motasem Sabbou.
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa michezo ya kundi D ambapo DR Congo itaavana na Mauritania kabla ya majirani Burundi kuvaana na Gabon katika mechi nyingine na kesho kuanza mechi za raundi ya pili kwa timu za kundi A kuonyeshana kazi.

No comments:

Post a Comment