STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 18, 2014

Kado achekelea, akiapa kung'ara zaidi duru la pili

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKEuWViBK1RvB2yszF1PxMhJ9oTDno9k9KRhyphenhyphennGjTRqcXKe0NrFPYNxFI7dlXI-3QjjBAfOVRNac5XEfoN6LD1rlraERS80n6_P6-mFCCORYMcAFnD-PqwN8vj-h31im-AGNf1Pg774b8/s640/shaaban+kado.jpg
Shaaban Kado 'Baba Munira'
KIPA wa kutaminiwa wa klabu ya Coastal Union, Shaaban Kado amesema anajisikia fahari kubwa kuweza kukaa langoni kwa muda wa dakika 1125 na kufungwa idadi ndogo ya mabao katika duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara,. huku akijitabiria kung'ara zaidi katika duru lijalo litakaloanza wikiendi hii.
 
Aidha kipa huyo aliyepo nchini Oman na kikosi cha timu yake kikifanya mazoezi kujiandaa na duru hilo la pili, amekiri duru lililopita lilikuwa lenye ushindani na kutabiria duru lijalo litakuwa gumu zaidi kutokana na usajili wa dirisha dogo na klabu zinavyojiandaa kwa sasa.
 
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya mtandao kutoka Oman, Kado alisema anajisikia fahari kubwa kuona amesimama kwenye milingoti mitatu ya klabu yake kwa mechi zote 13 akitumia dakika 1125 na kuifanya Coastal kuwa timu iliyofungwa idadi ndogo ya mabao katika duru lote la kwanza.
 
Kado alisema alicheza dakika zote 90 katika mechi 12 kabla ya mechi yao na Mbeya City kudaka kwa dakika 45 na kutoka kumpisha Said Lubawa aliyekuja kufungwa bao la kusawazisha la penati la Mbeya.
 
"Kwa kweli najisikia fahari sana kuona nimeidakia Coastal kwenye duru la kwanza karibu mechi zote na kufungwa mabao sita, nadhani duru lijalo kwa mazoezi ninayoendelea kuyafanya huku nitang'ara zaidi na kuipaisha timu yangu kwenye ligi," alisema Kado.
 
Kado alisema ligi ya msimu huu kwa ujumla imeonekana ngumu kutokana na ushindani uliopo na kukiri huenda duru lijalo likawa gumu zaidi kwa sababu timu zimepata nafasi yakupumzika na kurekebisha makosa yao kwa kusajili kwenye dirisha dogo na pia kujiandaa vyema wengine wakienda nje ya nchi.
 
Ukiondoa Coastal waliomaliza duru la kwanza katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 16 waliopo Oman, Yanga nao wamejichimbia Uturuki ikifanya mazoezi huku Kagera Sugar yenyewe ikijifua nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment