STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 18, 2014

Waamuzi 8 waula michuano ya CAF

WAAMUZI nane wa Tanzania wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC) zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.

Waamuzi hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.

Mujuni atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.

Naye Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa jijini Kinshasa.

Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.

No comments:

Post a Comment