STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 18, 2014

DR Congo wanyukwa kimoja CHAM 2014

http://mtn.ensight-cdn.com/content/RD-Congo-v-Libye-RD-Congo-T~1.jpg
DR Congo
 BAO pekee lililofungwa dakika ya pili na Erwin N'Guema Obame wa Gabon lilitosha kuizima DR Congo katika pambano la Kundi D la michuano ya Kombe la CHAN lililochezwa jioni hii.
N'Guema alifunga bao hilo akimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Samson Mbingui na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi huo na kuchupa hadi kileleni mwa kundi hilo kwa kufikisha pointi nne baada ya mchez wake wa awali dhidi ya Burundi kumalizika kwa sare pacha ya 0-0.
DR Congo yenyewe imesaliwa na pointi zake tatu ilizopata kwa kuilaza Mauritania ambayo baadaye itavaana na Burundi katika mchezo wa pili wa kundi hilo kuhitimisha mechi za raundi ya pili kwa makundi yote manne kabla ya mzunguko wa tatu kujua timu zitakazotinga robo fainali kufahamika rasmi.
Kwani mpaka sasa hakuna timu hiyo iliyojihakikisha kutinga hatua hiyo kutokana na timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo kubanana vilivyo japo nchi mbili za Msumbiji na Ethiopia zenyewe zimeshaaga mashindano kwa kufungashiwa virago baada ya kupoteza mechi zao mbili za awali katika makundi yao.

No comments:

Post a Comment