STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 24, 2014

Kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza kutimka wikiendi hii

Wazee wa Uturuki watakaovaana na Ashanti Utd kesho Taifa

Ashanti Unitrd weatakubali 5 nyingine kwa Yanga?
 MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar kutoka Morogoro.
Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi kati
ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
 
Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.

No comments:

Post a Comment