STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 24, 2014

TFF yaonya makocha, wasemaji wa timu kuhusu uchochezi

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha makocha na maofisa habari wa klabu za Ligi Kuu kujiepusha na kauli za chuki, uchochezi
na uongo kwa shirikisho na waamuzi kila timu zao zinapofanya vibaya kwenye mechi.

Ni wajibu wa makocha kuzungumzia matokeo ya timu zao kiufundi badala ya kushambulia waamuzi na TFF kwa maneno makali. 
 
Pia maofisa habari nao wanatakiwa kuwa makini katika kauli zao kuhusiana na matokeo na masuala
mengine.

Kwa wale watakaokwenda kinyume TFF itawafikisha kwenye vyombo vya kinidhamu na maadili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment