STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 20, 2014

Acheni Ronaldo awe Mwanasoka Bora wa Dunia

MABAO mawili aliyofunga juzi wakati akiivusha Real Madrid klwenye robo fainali, yamemfanya Cristiano  Ronaldo kufikia rekodi ya gwiji Ferenc Puskas ya kuifungia magoli katika klabu hiyo akiwabakisha wakali wengine watatu .
Ronaldo alifunga mabao hayo wakati wakiiangamiza  Schalke 04 na kumfanya Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka Bora wa Dunia kufikisha jumla ya mabao 242 katika mechi 236 - idadi sawa ya mabao kama gwiji huyo wa Hungary.
Ronaldo (29) ameifikia rekodi ya mabao ya Puskas akiwa amecheza mechi 25 pungufu ya gwiji huyo huku pia akiwa ameichezea klabu hiyo kwa miaka mitatu pungufu (mitano) ukilinganisha na Puskas (minane).
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno sasa anafukuzia rekodi ya ufungaji bora wa zama zote wa klabu hiyo, akiwa amewabakisha Santillana (aliyefunga magoli 290), Alfredo di Stefano (307) na Raul (323).
Nyota huyo bado ana nafasi ya kuvunja rekodi ya mabao kutokana na kiwango alichonacho na pia umri ukiw aunamruhusu huku akiwa na bahati ya kutokumbwa na majeraha ya mara kwa mara kama baadhi ya wachezaji nyota wengine.

No comments:

Post a Comment