STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 20, 2014

Robin van Persie 'aibeba' Man Utd, Borussia ikifa nyumbani kwao 2-1

Van Persie akifunga mkwaju wa penati
Kitu, Hulk akiifungia Zenit bao la kuongoza
MASHAMBULIAJI nyota wa Kiholanzi, Robin van Persie usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kuibeba Manchester United na kuivusha Roibo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bada ya kufunga hat trick wakiizamisha Olympiacos ya Ugiriki.
Manchester ambayo haikupewa nafasi kubwa miongoni mwa timu za England, ilipata ushindi huo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford na kufuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 kwani katika mechi ya kwanza walichezea kichapo cha mabao 2-0 ugenini.
Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, van Persie, alifunga utepe wa mabao kartika ya 25 kwa mkwaju wa penati kabla ya kuongeza jingine sekunde chache kabla ya mapumziko na kwa pasi ya Wayne Rooney na kuipeleka Mashetani Wekundu mapumziko wakiwa mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili wageni wakilisaka bao la kuwatibulia wenyeji, walishindwa kuhimili vishindo baada ya van 'Magoli' kuongeza bao la tatu dakia saba baada ya kuanza kipindi cha pili.
Katika mechi nyingine iliyochezwa nchini Ujerumani wanafainali wa mwaka jana wa michuano hiyo, Borussia Dotmund walijikuta wakichezea kichapo nyumbani chja mabao 2-1 dhidi ya Zenit.
Wageni waliwashtukiza Dotmund kwa bao la dakika 16 kupitia kwa Hulk kabla ya kuchomoa baadaye katika dakika ya 38 kupitia kwa Kehl aliyemalizia kazi ya Schmetzer na kufanya timu ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa hata jhivyo kipindi cha pili Zenith waliandika bao la ushindi kupitia Rondon.
Hata hivyo ushindi huo ulishindwa kuibeba Zenit kwa vile katika mechi ya kwanza nyumbani kwao walilala mabao 4-2, hivyo kuwapisha Wajerumani kufuzu robo fainali kwa jumla ya mabao 5-4.
Ratiba ya hatua hiyo kwa timu nane zilizofuzu inatarajiwa kutangazwa kesho, ingawa kuna hofu ya Chelsea kuangukia mikononi mwa Barcelona, Bayern Munich au Atletico Madrid.

No comments:

Post a Comment