STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 20, 2014

Casillas achekelea kuibania Yanga, ila alilia Mtibwa kupepesuka

KIPA tegemeo wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharrif 'Casillas' amesema pamoja na kufurahia kuibania Yanga na kuwalazimisha suluhu wakiwa pungufu uwanjani, bado hajaridhika na mwenendo wa timu yake na kuwataka wachezaji wenzake kupigana ili angalau imalize kwenye Top 4.
Casillas aliyekuwa mwiba kwa washambuliaji wa Yanga kwenye mechi iliyochezwa wiki iliyopita katika uwanja wa Jamhuri, alisema anajisikia faraja kuweza kuwanyiuma mabao nyota wa Yanga wakiongozwa na Emmanuel Okwi, Kiiza Hamis na Didier Kavumbagu,.lakini furaha yake ni kuona Mtibwa ikimaliza pazuri.
Kipa huyo wa zmaani wa Villa Squad alisema nafasi waliopo timu yao hailingani na hadhi ya ukongwe wake na kuwaomba wachezaji wenzake wakomae katika mechi zilizosalia kufungia msimu ili wamalize nadani ya Top 4.
"Nimefurahia kumbania tena Okwi na wenzake kama nilivyofanya wakati akiwa Simba na tulipokutana na watetezi hao msimu uliopita, lakini hii haisaidii kama tutaendelea kuporomoka kenye msimamo," alisema.
Alisema ni lazima wachezaji wa Mtibwa wapigane kuiwezesha timu yao kuwa kwenye nafasi za juu hata kama wameshapoteza nafasi ya kuwa mabingwa.
Mtibwa waliowahi kunyakua taji la ubingwa wa soka nchini kwa misimu miwili mfululizo mwaka 1999-2000 na 2000-2001, msimu huu imekuwa urojo kiasi cha kuondolewa kwenye mbiuo za ubingwa zilizobakia kwa timu za Azam, Yanga na Mbeya City.

No comments:

Post a Comment