Mwenyekiti
wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji amesema wanachama wanaopinga
maamuzi ya mkutano mkuu uliofanyika Juni Mosi 2014 katika Bwalo la
Polisi Osyterbay ya kuwaongezea muda wa mwaka mmoja, wafike makao makuu
ya klabu na kujiorodhesha majina yao kwa Katibu Mkuu.
Akiongea na waandishi wa habari
makao makuu ya klabu, Manji amesema sisi sote tunajenga nyumba hatuna
haja ya kugombania fito, wanaopinga maamuzi yale ni vyema
wakajiorodhesha majina yao ili kuweza kupata idadi yao na kama itafikia
idadi ya waliohudhuria mkutano ule watu 1522 basi tutaitisha mkutano
mwingine.
Vyombo vya Habari vimekua
vikiripoti kuwa baadhi ya wanachama hawakubaliani na maamuzi ya mkutano
mkuu, na mie ni mfuata Demokrasia namuagiza Katibu Mkuu kuweka reja hapa
makao makuu kwa siku 5 kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa 11 jioni hivyo
wale wote wanaosema/wanaopingana na maamuzi ya mkutano mkuu wapate
kujioorodhesha.
Pili kwa yoyote ambaye anaona
anaweza kuiongoza Yanga kwa sasa milango iko wazi, anaweza kufika makao
makuu na kuongea na katibu mkuu kisha anaweza kunadi sera zake/kuongea
na waandishi wa habari na baadae tutapeleka jina lake kwa Bodi ya
Wadhamini wakiridhika nitaitisha mkutano mkuu wa Uchaguzi.
Zoezi la kujiorodhesha
wanachama makao makuu litakua na usalama wa kutosha kutoka kwa jeshi la
Polisi ambapo patakua na askari wa usalama watakao kuwa wakilinda
usalama wa wanachama wanaofika kujiorodhesha kwenye reja hiyo.
Jumamosi ijayo Katibu Mkuu
atatoa ripoti ya idadi ya wanachama walijiorodhesha kwenye reja na kama
idadi ifikia 1522 kama ya waliohudhuria mkutano mkuu basi uongozi
utaitisha upya mkutano mkuu, na kama idadi yao haitafikia baadhi
demokrasia itatawala kwa kufuata maamuzi ya watu wengi.
Chanzo: Tovuti ya Yanga
No comments:
Post a Comment