STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 22, 2014

Jahazi la timu ya Babi Malaysia majanga matupu

BAADA ya kugangamala katika mechi yake iliyopita kwa kupata sare ya 2-2 ikitokea kupokea kipigo cha mabao 4-0 katika Ligi Kuu ya Malaysia, timu ya UiTM anayoichezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' imekutana na kiama baada ya kunyukwa mabao 8-0 na Felda United.
Hicho ni kipigo cha kwanza kikubwa kwa timu hiyo ikiwa na Babi aliyewahi kung'ara na timu za Yanga, Azam, Mtibwa Sugar, KMKM na Taifa Stars.
UiTM ilikumbana na pigo hicho uwanja wa ugenini wa Majlis Perbandaran, mjini Selayang baada ya Jumatatu iliyopita kupata sre ya 2-2 kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya PBAPP ikitokea ugenini kuchezea kichapo cha 4-0 toka kwa DRB-Hicom.
Katika mchezo huo wa juzi wakati UiTM ikizama kwa 8-0 magoli ya washindi yalifungwa naMohd Raimi katika dakika ya 20, Edward Junior Wilson aliyefunga mawili katika dakika ya  44 na 47 kabla ya Indra Putra Mahayuddin kufunga hat trick kwa magoli ya dakika za 62', 88' na 90 na mengine yakifungwa na '
Ndumba Makeche dakika ya  83' na Mohd Syahid Zaidon dakika moja baadaye.
Kwa matokeo hayo ya juzi, UiTM imeendelea kusaliwa na pointi 21 ikikamata nafasi ya 9 baada ya kushuka dimbani mara 21 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment