STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

Mashetani Wekundu chupuchupu wachinjwe nyumbani na Chelsea

Chelsea's Didier Drogba scores against Manchester United
Drogba akifunga bao la kuongoza la Chelsea
Manchester United's Robin Van Persie is denied by Chelsea's Thibaut CourtoisROBIN Van Persie ameiokoa timu yake ya Manchester United isife nyumbani baada ya kufunga bao la kusawazisha sekunde chache kabla ya pambano dhidi yao na Chelsea kumalizika kwenye uwanja wa Old Trafford.

Chelsea walionekana kabisa wamefanikiwa kuwaliza Mashetani Wekundu kwenye uwanja wao wa nyumbani na kuendelea ubabe, baada ya kutangulia kupata bao katika dakika ya 53 lililofungwa na Mshambuliaji nyota wa Ivory Coast, Didier Drogba.
Hata hivyo dakika za mwanzoni za nyongeza baada ya dakika 90 za mtanange huo kuelekea kumalizika Robin van Persie alifunga bao la kusawazisha kwa shuti la mguu wa kushoto na kulifanya pambano hilo kuisha kwa wababe hao kugawana pointi moja moja.
Chelsea ilijikuta ikimpoteza beki wake Branislav Ivanovic baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano kwa mchezo mbaya sekunde chache kabla ya mkwaju wa Van Persie kumaliza mzizi wa fitina katika pambano hilo ambao ulitawaliwa sehemu kubwa na wenyeji.

No comments:

Post a Comment