STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

Spurs yafa nyumbani, Eto'o, Lukaku waibeba Everton ugenini

Emmanuel Adebayor scores for Tottenham
Adebayor akifunga bao pekee la Spurs
Ayoze Perez
Ayoze Perez akishangilia bapo lake lililoiangamiza Spurs nyumbani kwao jioni ya leo
Samuel Eto'o
Samuel Eto'o akiifungia Everton bao
Romelu Lukaku
Lukaku akishangilia bao lake lililokuwa la pili kwa Everton
VIJOGOO vya London ya Kaskazini, Tottenham Hotspur wameendelea kuwa urojo kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kutandikwa mabao 2-0 na Newcastle United, huku Everton wakiifumua Barnley kwa mabao 3-1 ambapo mkongwe Samuel Eto'o alitumbukiza wavuni mabao mawili kati ya hayo.
Spurs ikiwa kwenye uwanja wake wa White Hartlane walianza mchezo huo kwa mbwembwe kwa kujipatia bao la kuongoza lililofungwa na Emmanuel Adebayor katika dakika ya 18 bao lilidumu hadi wakati wa mapumziko. Hilo lilikuwa bao la pili msimu huu kwa Nyota huyo wa Togo.
Kipindi cha pili kilianza kwa wageni kurejesha bao dakika ya 46 kupitia kwa Sammy Ameobi kabla ya Ayoze Perez kumaliza udhia kwa kufunga bao la pili na la ushindi katrika dakika ya 58 na kuwafanya Spurs kupokea kipigo cha pili mfululizo katika ligi hiyo bnaada ya awali kupigwa 4-0 na mabingwa watetezi, Manchester City wiki iliyopita.
Katika pambano jingine lililochezwa sambamba na hilo la White Hartlane, Everton ikiwa ugenini kucheza na Burnley ilipata ushindi wa mabao 3-1 huku Samuel Eto'o akifunga mabao mawili katika dakika ya 4 na 85 huku jingine likiwekwa kimiani na Romeo Lukaku dakika ya 29 na lile la wenyeji lilifungwa na Danny Ings. dakika ya 20.
Kwa sasa pambano la kukata na Mundu kati ya Manchester United dhidi ya wageni wao Chelsea ni mapumziko na milango yote ni migumu kwa maana hazijafungana.

No comments:

Post a Comment