Mbeya City |
Mtibwa Sugar |
Timu hiyo itawakaribisha Mtibwa inayoonekana kuwa fiti zaidi msimu huu katika pambano la kuhitimisha raundi ya tano wikiendi hii.
Mbeya City iliyoweka rekodi ya aina yake msimu uliopita kwa kupanda daraja na kumaliza msimu wakiwa nafasi ya tatu ilikuwa haijafungwa bao lolote wala kupoteza mchezo kabla ya mechi iliyopita dhidi ya Azam na kumfanya kocha Juma Mwambusi kukuna kichwa kuweza kurejesha makali ya kikosi chake kilichojijengea jina kubwa katika soka nchini.
Tofauti na msimu uliopita ambao walichuana na Azam kuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa hazijapoteza mchezo mpaka Yanga walipowatibulia, Mbeya City inalazimika leo kupata ushindi ili kujiweka pazuri katika mbio za kuwania ubingwa, ingawa Mtibwa Sugar ya msimu huu haitabiriki kwa kuwa na makali kama miaka iliyonyakua ubingwa mara mbili.
Mtibwa ambayo jana ilirejea kileleni mwa msimamo baada ya Azam kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu imetamba kuwa imeenda Mbeya kwa lengo moja tu la kushinda ili kuzidi kujiongezea pointi za kutwaa ubingwa msimu huu sambamba na kulipa kisai cha mabao 2-1 ilichopewa kwenye uwanja huo msimu uliopita.
Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime ametamba wameenda Mbeya kukusanya pointi kabla ya kuwasubiri Simba wiki ijayo watakaoumana nao uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mexime nahodha wa zamani wa Mtibwa na Taifa Stars, alisema suluhu waliyopata kwa Polisi hawakuifurahia, hivyo wanajipanga kuhakikisha wanapotezi tena pointi kizembe ili kutimiza lengo la kutwaa ubingwa msimu huu.
Kikosi hicho cha wakata miwa walianza msimu huu kwa kishindo kwa kuilaza Yanga mabao 2-0 kabla ya kuja kuifumua 'wageni' wa ligi hiyo Ndanda Fc kwa mabao 3-1 na kisha kuizima Mgambo JKT kwa bao 1-0 na kukusanya pointi 10 baada ya mechi nne, wakati wapinzani wao wana pointi tano kutokana na mechi nne walizocheza.
Mbeya City walianza kwa kutoka suluhu na JKT Ruvu kabla ya kuilaza Coastal Union bao 1-0 na kutoka tena suluhu ya Ruvu Shooting kabla ya kulala kwa Azam.
Katika mechi baina yao kwa msimu uliopita, Mtibwa na Mbeya Cirty zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyocjhezwa uwanja wa Manungu, Morogoro kabla ya Mbeya City kushinda mabao 2-1 uwanja wa Sokoine katika marudiano.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
P W D L F A GD Pts
01. Mtibwa Sugar 04 03 01 00 06 01 05 10
02. Azam 05 03 01 01 06 02 04 10
03. Yanga 05 03 01 01 07 04 03 10
04. Coastal Union 05 02 02 01 07 05 02 08
05. JKT Ruvu 05 02 01 02 04 05 -1 07
06. Ruvu Shooting 05 02 01 02 04 05 -1 07
07. Kagera Sugar 05 01 03 01 04 03 01 06
08. Mgambo JKT 05 02 00 03 02 04 -2 06
09. Prisons 05 01 02 02 05 05 00 05
10. Simba 05 00 05 00 05 05 00 05
11. Mbeya City 04 01 02 01 01 01 00 05
12. Stand Utd 05 01 02 02 03 08 -5 05
13. Ndanda Fc 05 01 00 04 07 10 -3 03
14. Polisi Moro 05 00 03 02 03 06 -3 03
No comments:
Post a Comment