STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

AS VITA YAJIWEKA PABAYA AFRIKA

http://congoplanet.com/pictures/news/as_vita_v_club_football_kinshasa_mubele_ndombe_z.jpg
AS VITA iliyong'ang'aniwa mjini KInshasa na ES Setif
KLABU ya AS Vita ya DR Congo imejiweka katika nafasi finyu ya kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani na ES Setif ya Algeria katika pambano la mkondo wa kwanza la Fainali za michuano hiyo.
Bao la mapema la kujifunga la Ndombe Mubele katika dakika ya 17 liliwaweka katika hali tete AS Vita kabla ya Lema Mabidi kusawazisha dakika za nyongeza kabla ya timu hizo kwenda mapumziko kwa mkwaju wa penati.
Kipindi cha pili wenyeji walishtukizwa tena kwa bao la pili la ES Setif lililofungwa katika dakika ya 58 na  Akram Djahnit.
Hata hivyo Mabidi alirudi tena kambani katika dakika ya 77 na kuwapa afueni wenyeji kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayopigwa Jumamosi ijayo nchini Algeria ambapo Wakongo hao watalazimika kupata ushindi ili kutwaa taji hilo baada ya kutwaa mara ya mwisho mwaka 1973 kati ya mara 14 ilizoshiriki michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment