STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

Mtibwa Sugar yatuma salamu Msimbazi, yaifumua Mbeya City 2-0

http://2.bp.blogspot.com/-bm4O4tF_oPg/VCrns2V90LI/AAAAAAAAy8g/QcCzcB7dMM8/s1600/MTIBWA%2BDHIDI%2BYA%2BYANGA.JPG
Mtibwa Sugar
MABINGWA wa zamani wa Tanzania, Mtibwa Sugar imeendeleza makamuzi yake katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya 'kutuma salamu' kwa vijana wa Msimbazi, Simba kufuatia kuitambia nyumbani kwao Mbeya City kwa kuicharaza mabao 2-0.
Mtibwa ilipata ushindi huo katika pambano pekee la Ligi Kuu lililochezwa leo kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeha na kufanikiwa kulipa kisasi cha mabao 2-1 ilichopewa na Mbeya City kwenye uwanja huo msimu uliopita.
Mabao ya Mtibwa inayonolewa na Nahodha wa zamani wa timu hiyo na Taifa Stars, Mecky Mexime, yaliwekwa kimiani na Ame Ali dakika ya 21 na jingine na mkongwe Vincent Barnabas na kuzidi kujichimbia kileleni ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.
Kipigo hicho kwa Mbeya City ni cha pili mfululizo baada ya wiki iliyopita kuadhibiwa kwa bao 1-0 na mabingwa watetezi, Azam na kuifanya timu hiyo iliyotamba msimu uliopita kusaliwa na pointi 5.
Mbeya iliyomaliza msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu kwa kishindo kwa kushika nafasi ya Tatu nyuma ya Azam na Yanga na mbele ya Simba na Kagera Sugar, imeshinda mechi moja tu na kuambulia sare mbili na kupoteza mech mbili.

No comments:

Post a Comment