STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

AS Vita katika vita ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Setif

http://3.bp.blogspot.com/-gfOtnWVkrS4/VChQY2vKN0I/AAAAAAAAPnY/wHKBhnwijdY/s1600/RDC%2BVita%2BClub%2BFinalista.JPG
Wenyeji AS Vita ya DR Congo
http://africafootballshop.com/wp-content/uploads/2014/09/ES-SETIF-ONZE-.jpg
ES Setif watakaoifuata As Vita mjini Kinshasa

KLABU ya AS Vita ya DR Congo leo inatarajiwa kushuka dimba la nyumbani kuanza kampeni yao ya kutwaa ubingwa wa Afrika wakati watakapoikaribisha ES Setif ya Algeria kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya fainali za michuano hiyo.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Tata Raphaël jijini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo).
AS Vita walipenya hatua hiyo baada ya miaka mingi kusikilizia kwenye bomba baada ya kupata ushindi wa kushangaza dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia kwa mabao 4-2 wakishinda nyumbani na ugenini mabao 2-1.
Wapinzani wao walitoshana nguvu na TOP Mazembe kwenye mechi ya Nusu fainali nyingine kwa kufungana mabao 4-4 na ES Setif kufuzu kwa faida ya bao la ugenini ambalo hata Rais wa FIFA Sepp Blater ametaka sheria hiyo iangaliwe upya na kurekebishwa.
Mazembe ilifungwa 2-1 ugenini kabla ya kushinda mabao 3-2 nyumbani kwa bao la jioni lililowanyima fursa wachezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kuweka historia ya kucheza fainali hizo kubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
AS Vita na Es Setif watarudiana tena wiki ijayo mjini Algers na kufahamika timu ipi ambayo itaibuka na taji hilo ambalo klipo wazi baada ya Al Ahly ya Misri kulitema mapema licha ya kuibania Yanga katika mechi ya raundi ya pili. Al Ahly ipo kwenye Kombe la Shirikisho ikiwania rekodi ya kuliwania taji hilo la pili kubwa.

No comments:

Post a Comment