STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 26, 2014

Juventus yatamba, Chievo Verona yapigwa Italia nyumbani,

Arturo Vidal scores
Vidal Arturo akifunga bao la kwanza la Juventus
MABAO mawili kupitia kwa nyota wake, Arturo Vidal na Llorente yameipa ushindi muhimu Juventus katika Ligi Kuu ya Serie A nchini Italia dhidi ya Palermo, huku Chievo Verona wenyewe wakifa nyumbani kwa mabao 2-1 kw Genoa.
Nyota kutoka Chile, Vidal aliiandikia 'Kibibi cha Turin' bao dakika ya 32 akimalizia kazi nzuri ya Carlos Tevez kabla ya Llorente kuja kuongeza bao la pili katika kipindi cha pili dakika ya 64 na kuifanya Juve kufikisha jumla ya pointi 22 baada ya mechi nane.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Chievo walilala mabao 2-1 nyumbani mbele ya wageni wao Genoa, huku Udinese wakishinda mabao 2-0 dhidi ya Atalanta waliowafuata kwao.
Michezo mingine ya ligi hiyo inaendelea kuchezwa kwa sasa uwanjani.

No comments:

Post a Comment