STRIKA
USILIKOSE
Sunday, October 26, 2014
Man Utd, Chelsea hataposhi leo, Spurs kujiuliza kwa Newcastle
KIVUMBI cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea leo kwa mechi tatu, ambapo 'Mashetani Wekundu' watakuwa uwanja wa nyumbani wa Old Trafford kuwakaribisha vinara wa ligi hiyo, Chelsea.
Chelsea inaifuata Manchester United ikiwa na hamasa ya ushindi mnono wa mabao 6-0 iliyopata Jumanne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya timu ya Maribor.
Manchester waliotoka kulazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya West Bromwich Albion itaisubiri Chelsea ikiwa na amani baada ya nyota wake, Angel di Maria kuwa fiti kwa ajili ya kuwavaa vijana wa Jose Mourinho.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa hivi karibuni akitokea Real Madrid alishindwa kumaliza pambano lililopita na kuleta hofu kwamba atalikosa pambano hilo kabla ya wiki hii klabu hiyo kuwatoa wasiwasi mashabiki baada ya kufanyiwa vipimo vya afya na kuonekana tatizo lake siyo kubwa.
Hata hivyo Mashetani Wekundu wanaokamata nafasi ya sita katika msimamo wakiwa nyuma ya pointi 10 kwa Chelsea itamkosa nahodha wake, Wayne Rooney na Jesse Lingard walio majeruhi, huku Chelsea wenyewe haitakuwa na mfumani nyavu wao anayeongoza orodha ya wafungaji katika ligi hiyo, Diego Costa na John Obi Mikel walio majeruhi.
Hata hivyo Morinho, alinukuliwa mapema jana kuwa huenda akamtumia Coast katika mechi ya leo, huku akisisitiza kuwa silaha kubwa kwake ni Didier Drogba ambaye ana nguvu na kujua kufunga kama alivyofanya wakati wakiizamisha Maribor kwa mabao 6-0.
Chelsea inayoongoza msimamo ikiwa na pointi 22, itawakosa pia Andre Schurrle na Azpilicueta wanaotumikia adhabu ya kadi nyekundu, ingawa bado ina nyota kadhaa ambao wanatarajiwa kuibeba mbele ya wapinzani wao.
Rekodi zinaonyesha kwa misimu miwili mfululizo, Mashetani Wekundu hawajawahi kupata ushindi dhidi ya Chelsea hali inayofanya pambano hilo kuwa na mvuto wa aina yake kutaka kujua kama Manchester itafuta uteja au la.
Pia leo kutakuwa na michezo mingine miwili ambapo Tottenham Hotspur iliyofumuliwa mabao 4-0 wiki iliyopita na watetezi Manchester City itakuwa nyumbani kuwakaribisha Newcastle na Everton itawafuata waliopanda daraja msimu huu Burnley.
Mechi hizo zote zitachezwa mapema mchana kabla ya pambano la Manchester United na Chelsea watakaovaana jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment