STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 6, 2014

FifPro yatishia kugomea Fainali za Kombe la Dunia za Qatar

http://s1.reutersmedia.net/resources/r/?m=02&d=20110914&t=2&i=500889270&w=580&fh=&fw=&ll=&pl=&r=img-2011-09-14T173158Z_01_NOOTR_RTRMDNC_0_India-593363-1
UMOJA wa Wachezaji wa Kulipwa FIFPro, umetishia kuigomea michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022 nchini Qatar.
Kiongozi wa umoja huo, Theo van Seggelen amesema kuwa wachezaji wanaweza kugomea kushiriki michuano hiyo iwapo itaendelea kushinikizwa kuchezwa katika majira ya kiangazi.
Joto katika nchi hiyo ya barani Asia hufikia hadi nyuzi joto 40 katika kipindi cha kati ya mwezi Mei na Septemba, ingawa muda haswa wa kufanyika michuano hiyo bado haujapangwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA.
Van Seggelen amesema Fifpro haitawaruhusu wachezaji kuhatarisha afya zao kwa kushiriki fainali hizo ambazo zimeleta mzozo tangu zilipotangazwa na shirikisho la sokla duniani, FIFA miakla michache iliyopita.
Aliongeza kwa kudai kuwa kama ikibidi anaweza kulipeleka suala hilo mahakamani ili kupata haki ya msingi.
Kiongozi huo amesema ana uhakika FIFA haitaweza kupingana na washauri wao wenyewe wa masuala ya afya kwa kuruhusu michuano hiyo kuchezwa majira ya kiangazi.
Van Seggelen pia aliponda ombi la vilabu vya Ulaya kutaka michuano hiyo kufanyika katika kipindi cha Aprili na Mei akidai kuwa halina mashiko kwani bado kipindi hicho kinaweza kuhatarisha afya za wachezaji.

No comments:

Post a Comment