STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 6, 2014

Ndege ya Rais wa China yadaiwa kutorosha nyara za Tanzania


Rais Xi JinPing wa Uchina alipozuru Tanzania mwaka uliopitaINADAIWA kuwa, Ndege ya Rais wa China, aliyekuwa ziarani nchini Tanzania mwaka uliopita ilihusija kutorosha nyara za taifa zikiwamo Pembe za Ndovu.
Inaelezwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za Pembe za Ndovu Tanzania kisha kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping, wakati alipozuru bara Afrika. 
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London. 
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini Tanzania mwaka uliopita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa. 
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu. 
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Hata hivyo serikali imekanusha taarifa hizo za kuwepo kwa biashara ya Pembe za Ndovu nchini.
Msemaji wa serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Mwambene amesema serikali ya Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara haramu ya meno ya tembo kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na China.
Serikali imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa kichina wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya meno ya tembo.
BBC  

No comments:

Post a Comment