STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, November 6, 2014

Watatu kati ya waliokufa ajalini Ifakara watambuliwa!

http://api.ning.com/files/st-pA-4csCGQ4-t4jx12MikAxzFvyvUW-zC35WxKpbGhYiXhPqU4H5di0w8j4TwMDjoHYFJKlkEAnto0riRQW1TncFQ-7kLz/5ajali5.jpg
Mabaki ya basi la Al Jabir (Picha zote na Global Publishers)
 

Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
Basi hilo likiwa limepinduka.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.
MIILI ya watu watatu kati ya 12 waliofariki katika ajali mbaya ya gari dhidi ya treni huko Ifaraka mchana wa leo imetambuliwa.
Watu hao walifariki dunia papo hapo na wengine 45 kujeruhiwa baada ya basi walililokuwa wakisafiria la Kampuni ya Al Jabir kugonga treni eneo la Kiberege Ifakara Wilaya ya Kilombero.
 Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema basi hilo lilokuwa likitokea Morogoro- Ifakara kugonga Treni ya Tazara iliyokuwa ikitokea Mbeya – jijini Dar es Salaam.
 Kamanda huyo  aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.
 Kamanda Paulo alisema chanzo cha ajali hiyo ni  dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T725 ATD Scania, alivuka barabara yenye makutano na reli bila ya kuchukua tahadhani na hivyo kuigonga treni.
Alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mtakatifu Fransis Ifakara na kituo cha afya Kibaoni kwa ajili ya matibabu.
Kamanda Paulo alisema miili ya marehemu nayo imehifadhiwa katika hospitali ya mtakatifu Francis Ifakara.
Alisema dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment