STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 30, 2013

Rais CAF ampongeza Malinzi kwa ushindi TFF

Rais wa CAF, Issa Hayotou
Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.
Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.
Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.

Simba, Kagera Sugar kesho hapatoshi Dar

Kagera Sugar
Simba
 LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya 12 kesho kwa pambano kati ya Simba na Kagera Sugar, mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar  es Salaam.
Pambano hilo ni fursa kwa Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi japo kwa muda, kwani iwapo atashinda itafikisha pointi 23 na kulingana nma vinara wa sasa Azam na Mbeya City.
Katika mechi yao iliyopita Simba ilikula kichapo kwa Azam kwa mabao 2-1 na kuwatoa kileleni, hivyo huenda kesho itaikaribisha Kagera kwa hasira ili kuweza kurudi kwenye ufalme wake kabla ya kusubiri kuangalia watani zao Yanga watafanya nini Ijumaa watakapovaana na JKT Ruvu.
Mshambuliaji nyota Amissi Tambwe ambaye hakucheza katika pambano lililopita na kumpa wakati mgumu 'pacha' wake, Betram Mombeki inaelezwa huenda akashuka dimbani kesho na kuendeleza kazi yake ya mabao ili kumkimbia Hamis Kiiza 'Diego' wa Yanga aliyemfikia jana baada ya kufunga bao Yanga ilipoilaza Mgambo JKT mabao 3-0.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Tuesday, October 29, 2013

Bale, Ronaldo, Messi kuchuana tuzo ya FIFA's Ballon d'Or

Bale na Ronaldo
Zlatan Ibrahimovic

MCHEZAJI ghali kwa sasa Gareth Bale, ni miongoni mwa wachezaji 23 akiwamo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi watakaowania Tuzo ya FIFA cha Mchezaji Bora Duniani  (FIFA's Ballon d'Or).
Aidha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, Jose Morinho wa Chelsea na Alex Ferguson ni kati ya makocha watakaowania tuzo ya Kocha Bora wa Dunia wa FIFA.
Winga huyo (23) amejumuisha katika orodha ya awali ya watakaowania tuoz hiyo inayotolewa kila mwaka ambayo kwa sasa inashikiliwa na Messi.
Mkali huyo aliteua Real Madrid msimu huu akitokea Tottenham Hotspur, alivunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye uhamisho ghali akipiku rekodi ya Ronaldo kwa kunyakuliwa na Madrid atapigana kumbo na Mchezaji Bora wa Ulaya, Franck Ribery.
Orodha kamili iliyotangazwa na FIFA kuwania tuzo hiyo ni kama ifuatavyo;
Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris Saint-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer, (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).
Orodha kamili ya makocha watakaochuana katika tuzo hizo za FIFA ni pamoja na  Carlo Ancelotti (Paris Saint-Germain), Rafael Benitez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente del Bosque (Spain), Alex Ferguson (formerly Manchester United), Jupp Heynckes (formerly Bayern Munich), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal)