STRIKA
USILIKOSE
Thursday, May 17, 2012
Cheka ajipanga kumtoa nishai Mzambia
BINGWA mpya wa IBF Afrika, Francis Cheka 'SMG' ametamba kwamba hatawangusha Watanzania katika pambano lake la kutetea taji hilo dhidi ya Mzambia, Stephen Chungu atayepigana nae Julai mwaka huu.
Cheka, alisema kwa kutambua umuhimu wa pambano hilo anatarajia kuingia kambini mapema zaidi ili kujiweka fiti kabla ya kuvaana na Chungu katika pambano la uzani wa Super Middle la raundi 12.
Awali Cheka alikuwa apambane na Mohammed Akpong wa Ghana, lakini kutokana na masharti aliyoyatoa bondia huyo, imemfanya waratibu wa IBF kumbadilishia Mzambia huyo mwenye rekodi ya kucheza michezo 16.
"SItaki kuwaangusha Watanzania na hivyo nitaanza mapema kambi yangu ili kumkabili nikiwa fiti na kuhakikisha napata ushindi hiyo Julai," alisema.
Cheka anayeshikilia pia mataji ya Kamisheni ya Ngumi Dunia, WBC, ICB na UBO, alisema ushindi wake dhidi ya Mada Maugo uliomfanya atwae taji hilo la IBF Afrika imekuwa kama chachu ya kuzidi kusaka mafanikio kimataifa.
"Akili yangu kwa sasa ni kusaka mafanikio zaidi duniani, ndio maana sitaki kufanya uzembe wa aina yoyote katika pambano langu lijalo na mengine ya kimataifa ambayo ndiyo yenye ulaji mkubwa," alisema.
Cheka alitwaa taji hilo kwa kumshinda Mada Maugo aliyekacha ulingo wakati wakijiandaa kwa raundi ya saba kwa kile alichodai alikuwa akiona 'kiza' na kumfanya bingwa huo wa IBF kushinda pambano la 11 mfululizo tangu 2008.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment