basi lililopata ajali nchini Italia (Picha:AFP) |
WATU wapatao 38 wamepoteza maisha yao huku wengine wakikimbizwa hospitali kwa matibabu kutokana na ajali ya basi iliyotokea nchini Italia.
Waokoaji wa Kusini kwa nchini hiyo wamesema watu hao walikuwa katika basi hilo walilokuwa wakisafiria lililotumbukia ndani ya mtaro wenye urefu wa mita 30.
Baadhi ya abiria waliokimbizwa hospitalini kwa matibabu hali zao zinaelezwa kuwa mbaya kwa majeraha waliyoyapata katika ajali hiyo.
Inaelezwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria waliokuwa wakirudi mjini Napoli kutoka jimbo la kusini la Campania.
Haijabainika chanzo cha ajali hiyo iliyohusisha pia magari kadhaa na kwamba basi hilo lililokuwa limebeba abiria 50 wakiwamo watoto waliokuwa wanatoka Naples baada ya kufanya hija.Basi hilo liligonga magari kadhaa kabla ya kuanguka ndani ya mtaro mjini Avellino.
Picha zilionyesha miili ya watu iliyokuwa imetapakaa kando ya barabara pamoja na magari yaliyokuwa yameharibiwa kwenye ajali hiyo.
Dereva wa basi hilo ni miongoni mwa wale waliofariki.
Waathiriwa kadhaa hata hivyo hawakuweza kutambulika , kwa mujibu wa msemaji wa polisi akisema kuwa wangali wanatoa miili katika magari yaliyoharibiwa.
Ajali hiyo ya Italia imekuja siku chache baada ya watu wengine zaidi ya 70 kufa katika ajali mbaya ya Treni ya kwenda kasi iliyokea Kaskazini Magharib ya Hispania wiki iliyopita.
BBC
No comments:
Post a Comment