STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 1, 2013

APR, Vital'O katika fainali ya aina yake Darfur


http://upload.wikimedia.org/wikipedia/en/f/fe/Vital%27O_FC_logo.png


http://en.starafrica.com/football/files/2012/11/APR-logo.jpg


TIMU ya APR ya Rwanda leo inatarajia kukutana na majirani zao Vital'O ya Burundi katika mechi kali ya fainali ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) itakayofanyika kwenye Uwanja wa El Fasher ulioko Darfur Kaskazini nchini Sudan.
Timu hizo pinzani ambazo mwaka huu zilikutana katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika na Vital'O kusonga mbele, zilikutana kwenye hatua ya makundi na kutoka sare ya goli 1-1 huku APR ikitangulia kupata bao na Warundi kusawazisha.
Wanyarwanda APR wamefika hatua hiyo baada ya kuwafunga wenyeji El Merreikh  El Fasher kwa penati 3-1 kufuatia sare ya 1-1 waliyomaliza katika dakika 120 huku Vital'O wakifuzu kwa hatua ya fainali leo baada ya  kuwafunga mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Rwanda, Rayon Sports bao 1-0.
APR ambayo sasa iko chini ya kocha kutoka Ujerumani, Andreas Spier, inasaka ubingwa wa nne wa mashindano hayo. Mara ya mwisho walibeba taji la michuano hiyo inayofadhiliwa na rais wa nchi yao mwaka 2010 na wapinzani wao  Vital'0 hawajawahi kutwaa kombe hilo.
Bingwa wa leo atajinyakulia zawadi ya kwanza ya dola za Marekani 30,000 (Sh. milioni 48) huku mshindi wa pili akiwa na uhakika wa  kuondoka na dola za Marekani 20,000 (Sh. milioni 32).
Katika hatua nyingine, leo jioni kutakuwa pia na mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambapo wenyeji El Merreikh El Fasher watavaana na Rayon Sports kwenye uwanja huo huo wa El Fasher.
Yanga ya Tanzania Bara ndiyo inashikilia ubingwa wa mashindano hayo lakini ilishindwa kwenda kutetea taji lake mjini Darfur kufuatia amri ya serikali ya Tanzania kuzuia timu zake kwenda kwenye michuano hiyo kwa sababu za kisalama. Hata hivyo, serikali ilibaini baadaye kuwa hali ya Darfur ni shwari, lakini ruhusa yake haikuzisaidia timu za Tanzania za Yanga, Simba na Falcon ambazo nafasi zao zilishatwaliwa na timu nyingine.

No comments:

Post a Comment