Brazil wakishangilia taji lao la ubingwa wa Mabara baada ya jana kuitafuna Hispania kwa mabao 3-0 |
Fred akishangilia moja ya mabao yake mawili huku mfungaji mwingine Neymar akimfuata kwa nyuma kushoto |
Hispania ambao licha ya taji la dunia, pia inashikilia ubingwa wa nchi za Ulaya na jana ilikuwa ikiota kuongeza taji jingine la Mabara, lakini wakajikuta wakikumbana ana kipigo hicho toka kwa Brazili ambao wameanza kurejesha makali yao baada ya kuzorota miaka ya hivi karibuni na kufikwa na nchi za Ulaya.
Katika mchezo huo, mabingwa wa Dunia na Ulaya walipoteza mchezaji mmoja na pia wakashindwa kufunga Mabao ya Fred aliyefunga mawili na Neymar yalitosha kuizima Hispania iliyoing'oa Italia katika nusu fainali ya michuano hiyo ambayo katika mchezaji wa jana ilimpoteza Gerrard Pique na kukosa pia penanti iliyopoteza na Sergio Ramos.
Fred alifunga bao la kwanza dakika ya pili kabla ya Neymar akafunga bao la pili dakika moja kabla ya mapumziko na Fred anaongeza jingine dakika mbili baada ya kuanza kipindi cha pili na kuwafanya wenyeji kushangilia taji la tatu mfululizo la michuano hiyo.
Brazil imetwaa taji hilo kwa mara nne mara ya kwanza mwaka 1997 michuano ilipofanyika nchini Saud Arabia kabla ya kutwaa tena mwaka 2005 nchini Ujerumani, kisha kunyatua tena nchini Afrika Kusini katika fainali za mwaka 2009 na jana ikaongeza tena ikiwa nchi mwenyeji.
Katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo, Italia ilijifariji kwa kunyakua nafasi hiyo kwa kuilaza Uruguay kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 kwa kufungana mabao 2-2.
Katika hatua hiyo ya penati Italia walipata penati 3 dhidi ya mbili za Uruguay ambao walikuwa na kazi ya kurudisha mabao katika muda wa kawaida kupitia kwa Edinson Cavani.
No comments:
Post a Comment