STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 1, 2013

Gor Mahia, Bandari zashindwa kutambiana Kenya

Wachezaji wa Bandari, Gor Mahia wakiumana uwanjani (Picha Super Sport)
 MABINGWA wa zamani wa Kenya na Kombe la Washindi Afrika, Gor Mahia ya Kenya jana ilifanikiwa kukwea hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya kulazimishwa suluhu na Bandari Mombasa katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa City, jijini Nairobi.
Mahia kwa suluhu hiyo imeipumulia Bandari waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 24 kwa tofauti ya pointi moja kwani vigogo hao wana pointi 23 na ikiwa na michezo miwili mkononi wakati ligi ikiwa raundi ya 15.
Katika pambano hilo lililokuwa likitangazwa na kituo cha redio cha Citizens ya Kenya, Gor Mahia itajilaumu kwa kukosa mabao mengi ya wazi mbele ya wageni wao ambao wanatenganishwa na vinara wa ligi hiyo ya Kenya Thika United kwa pointi mbili. Thika ambayo itashuka dimbani jioni ya leo kuumana na AFC Leopards ugenini inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 26 ikicheza mechi 14.
Suluhu hiyo ya jana nyumbani ni ya pili kwa Gor Mahia kwani kabla ya pambano hilo na Bandari ililazimishwa sare kama hiyo na Thika United.

No comments:

Post a Comment