STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 15, 2013

Manchester United sasa yamgeukia Fabregas

Cesc Fabregas
 BAADA ya kumkosa kiungo Thiago Alcantara aliyetimkia kwa Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, klabu ya Manchester United imeelekeza shabaha yake kwa kiungo wa zamani wa Arsenal anayeichezea Barcelona, Cesc Fabregas.
Mashetani Wekundu hao, wameamua kuweka mezani kitita cha pauni 26 ili kumnasa nyota huyo wa Hispania ili atue Old Trafford.
United imepania kumnasa mkali huyo ikichuana na Arsenal ambao pia wameonyesha nia ya kumrejesha kiungo huyo Emirates baada ya kumuuza miaka miwili iliyopita kwa dau la pauni milioni 31.
Ofa iliyotangazwa na United kwa Fabregas ni pungufu ya kiasi cha Pauni Milioni 5 kufika dau la Pauni Mil 30.75 inayoendelea kushikilia rekodi ya mchezaji wa bei ghali kusajiliwa OT ilipomnunua mshambuliaji wa Tottenham, Dimitar Berbatov mwaka 2008. 
Duru za soka zimekuwa zikisema kuwa kuna uwwezekano mkubwa kwa Cesc kurejea Arsenal licha yha kwamba mwenyewe alishanukuliwa kwamba angependa kuendelea kuichezea Barcelona kwa vile anafurahia kuwepo hapo ili kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu.
Kama atatua kwa United, kutamfanya nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kuungana tena na mchezaji wenzake wa zamani wa Emirates Robin van Persie ambaye alihama klabu hiyo na Arsena msimu uliopita na kufanikiwa kutwaa nao taji la ubingwa wa EPL.

No comments:

Post a Comment