STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 15, 2013

Mbishi Real ataka watanzania kuutakaa udini

Mbishi Real katika pozi
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Fred Kaguo 'Mbishi Real' ameibuka na kampeni mpya ya kuwahamasisha watanzania kuepuka vitendo vya kibaguzi vya udini na ukabila iitwayo 'Tanzania Tuukatae Udini'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mbishi anayetamba na nyimbo kadhaa ikiwamo 'Tozi wa Mbagala' alisema kampeni hiyo ni maalum kwa kutaka kuwakumbusha Watanzania kuwa wote ni wa moja na hakuna aliye bora zaidi ya wengine.
"Hakuna asiyejua hali inayoendelea nchini kwa sasa japo ni kwa chinichini, hivyo kama msanii nimeona nitumia kipaji changu kuwahamasisha watanzania wenzangu kuukata udini ili kutovunja umoja wetu tuliokuwa nao kwa muda mrefu," alisema.
Mbishi alisema kampeni hiyop ambayo kwa sasa inatafutiwa wadhamini ili kuanza rasmi baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani utafanyika nchini nzima kwa kushirikisha maonyesho mbalimbali ya sanaa ikiwamo nyimbo toka wa wasanii na makundi tofauti.
"Ni kampeni niliyopanga kuifanya nchi nzima kuwahamasisha wenzangu na itaambatana na burudani mbalimbali, kwa sasa najiandaa kupeleka maombi serikalini na kwa wafadhili ili kufanikisha vyema kilichjokusudiwa kwenye kampeni hiyo," alisema Mbishi.
Mbishi alisema matrukio machache yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya nchi yenye kuhusiana na masuala ya kidini kama yale ya kugombea kuchinja na milipuko ya mabomu kanisani na kukojolewa na kuchanwa kwa Qur'an ni dalili mbaya kwa Tanzania yenye amani.


No comments:

Post a Comment