STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 15, 2013

Polisi Tanga wanasa kete za dawa za kulevya

Baadhi ya dawa za kulevya vinazonaswa nchini
WIMBI la biashara ya dawa za kulevya linazidi kushika kasi baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kukamata kete 46 za dawa za kulevya aina ya Cocaine baada ya kufanya msako kwenye maeneo yanayosadikiwa wanakaa watumiaji wa dawa hizo wilayani Pangani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe, alisema jana kuwa dawa hizo zilikamatwa Jumatano iliyopita baada ya polisi kuvamia eneo hilo na kuwakamata watumiaji wanne.
Alisema polisi walifanikiwa kukamata dawa hizo kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema.
Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kuwa ni Shaban Ramadhan (20), mvuvi na mkazi wa Malindi wilayani Pangani, Mohamed Kijiba, mkazi wa Fungoni na Iddi Hamdan (21), mkazi wa Fungoni mjini Pangani ambao wote ni wavuvi.
Kwa siku za karibu janga la dawa za kulevya limezidi kushika kasi na kuonyesha wazi 'vita' dhidi ya dawa hizo ni kama hazizai matunda kutokana na kila uchao kunaswa 'unga' ambao huingizwa nchini toka ng'ambo.

No comments:

Post a Comment