KLABU ya Arsenal bado haijakata tamaa na nia yake ya kumng'oa mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez kutoka Liverpool kwa kudaiwa ipo tayari kuongeza dau hadi kufikia pauni Mil. 35 mradi iimnyakue mkali huyo wa mabao.
Suarez amekuwa chaguo la kwanza la kocha Arsene Wenger katika usajili wa majira ya joto na iko tayari kutoa dau zaidi ya ile ya awali ya pauni Mil.30 iliyokataliwa na Liverpool wanaotaka angalau pauni Mil 40.
Klabu hiyo ya London ya Kaskazini inachuana na Manchester City na Real Madrid zinazomfukizia pia 'mtukutu' ambaye amekuwa na wakati mgumu nchini England kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari hasa kwa kadhia zake tata za hivi karibuni katika EPL.
Wenger amekuwa akimhitaji mshambuliaji huyo huku pia akimwinda Higuian Gonzalo ambaye bado haijafahamika kama itakuwa naye katika msimu ujao baada ya kuelezwa amejiunga na timu yake ya Real Madrid kuanza mazoezi.
Hata hivyo kuna kila dalili Arsenal kumnasa mshambuliaji huyo wa Argentina na iwapo itafanikiwa kuishawishi Liverpool kumuachia Suarez itakuwa imelamba dume baada ya kuwa misimu karibu nane isiyo na tija yoyote England na kimataifa.
No comments:
Post a Comment