Cristiano Ronaldo |
Gareth Bale, anayetajwa kuwa bado kidogo tu atue Real Madrid |
Madrid,
Hispania
KLABU
ya Real Madrid inaamini kwamba, sasa ipo hatua za mwisho za kukamilisha
uhamisho wa winga wa Tottenham, Gareth Bale baada ya kuanza kujiandaa kutoa
pauni milioni 87 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 209.3 za Tanzania.
Baada
ya wiki nzima Spurs kusisitiza kwamba, Bale hauzwi, sasa Klabu hiyo ya White
Hart Lane imenywea na tayari Real inajipanga kutoa dau hilo ambalo litaweka
rekodi ya dunia kwa uhamisho wa wachezaji.
Sportsmail
limeeleza kuwa linatambua wazi kuwa kikanuni, tayari Spurs imekubali dau hilo,
lakini litamthibitisha mchezaji huyo kwa Real Madrid pale tu litakapopata
mrithi wake.
Katika
kujipanga upya, tayari Spurs inatarajia kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa
Valencia, Roberto Soldado kwa dau la pauni milioni 26 (sh. bilioni 62.5 za
Tanzania) ambapo pia Kocha Andre Villas-Boas anataka kumng'oa Alvaro Morata
katika Uwanja wa Bernabeu ikiwa ni sehemu ya kumwachia Bale.
Morata,
20, anayecheza safu ya ushambuliaji, huku akiwa ameshakifungia mara mbili
Kikosi cha Wakubwa cha Real, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora kwa siku
zijazo.
Spurs
inataka kuisisitiza Real Madrid kuwa Morata awe sehemu ya makubaliano ya wao
kumwachia Bale.
Morata
alikuwa kinara wa ufungaji kwenye michuano ya Ulaya ya wachezaji wenye umri
chini ya miaka 21 (Euro U-21), ambayo ilifanyika Israel mwaka huu, baada ya
kufunga jumla ya mabao manne na kuiwezesha Hispania kutwaa kombe.
Endapo
Spurs itaridhia kumuuza Bale kwa pauni milioni 87, atakuwa amevunja rekodi ya
dunia iliyowekwa na Cristiano Ronaldo, aliyetua Real Madrid kwa pauni milioni
80 akitokea Manchester United 2009.
Nyota
anayefuata kwa kuuzwa ghali ni Zlatan Ibrahimovic, aliyetua Barcelona 2009,
akitokea Inter Milan kwa pauni milioni 56.5. Kaka anafuata kwa pauni milioni 56
kutoka AC Milan kwenda Real Madrid (2009).
No comments:
Post a Comment