STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 2, 2013

TFF yatoa shushu ya usajili wa wachezaji

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya usajili wa wachezaji nchini kwa msimu mpya kwa siku mbili zaidi tofauti na ivyokuwa imepangwa awali.

TFF ilitangaza awali kwamba mwisho wa usajili huo wa wachezaji ungekuwa Agosti 3 yaani kesho badala yake umetangaza kwamba utafungwa rasmi Jumatatu (Agosti 5). 

Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.

Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.

Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom

No comments:

Post a Comment