STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 2, 2013

Sikinde kula Idd Dar, Bitchuka anatabasamu tamu

Hassani Bitchuka akiimba kando ya Adolph Mbinga

Baadjhi ya waimbaji wa Sikinde, Hassani Kunyata, Abdallah Hemba na Hassani Bitchuka
BENDI kongwe wa muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' imekamilisha mipango ya kuingia studio kurekodi nyimbo tano zilizosalia, huku ikitangaza ratiba yao ya sikukuu ya Eid el Fitri ambapo imesema Idd zote tatu watakuzila wakiwa jijini Dar es Salaam.
Aidha mwanamuziki wao mkongwe, Hassani rehani Bitchuka ameibuka na wimbo mpya uitwao 'Tabasamu Tamu' ambao unatarajiwa kutambulishwa rasmi katika maonyesho hayo ya sikukuu ya Idd.
Katibu wa bendi hiyo, Hamis Milambo aliiambia MICHARAZO kuwa wapo katika hatua ya mwisho kabla ya kuingia studio za Sound Crafters ili kurekodi nyimbo hizo kati ya sita za albamu mpya iitwayo 'Jinamizi la Talaka'.
Milambo alisema baadhi ya nyimbo hizo zilianza kupigwa kwenye maonyesho ya bendi hiyo kabla haijaingia mapumzikoni kupisha mfungo wa Ramadhani unaoelekea ukingoni.
"Tunafanya mipango ya kuingia studio hivi karibuni ili wakati wa Idd  albamu iwe imekamilika na ni nyimbo tano kati ya sita ndizo zitakazorekodiwa kwa vile 'Jinamizi la Talaka' yenyewe ilisharekodiwa na inaendelea kutamba hewani," alisema Milambo.
Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni 'Nundu ya Ng'ombe' uliotungwa na mcharaza gitaa la solo wao, Ramadhani Mapesa 'Dolar Dolar', 'Za Mkwezi' wa Abdallah Hemba, 'Deni Nitalipa' na 'Kukatika kwa Dole Gumba' za nyota wao Hassain Rehani Bitchuka 'Stereo' na 'Kibogoyo' uliotungwa kwa ushirikiano wa wanamuziki wote wa Sikinde.
Juu ya ratiba yao ya sikukuu ya Eid, Milambo alisema safari hii wameamua kula sikukuu hiyo na mashabiki wao wa jijini Dar es Salaam.
Alisema Idd Mosi watakamua kwenye ukumbi wa TCC Chang'ombe kabla ya Idd Pili kufanya maonyesho yao katika ukumbi wa Pentagone Pub uliopo Mivinjeni Kurasini na kumalizia burudani yao itakayoenda sambamba na utambulisho wa wimbo wa Tabasamu Tamu uliotungwa na Bitchuka Magereza Ukonga.

No comments:

Post a Comment